Katibu mkuu wa UM atoa mwito wa kukomeshwa kwa uhasama kwenye eneo la Tigray, Ethiopia
2022-10-18 08:01:28| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa mwito wa kukomeshwa kwa vitendo vya uhasama kwenye eneo la Tigray nchini Ethiopia ikiwa ni pamoja na kuondolewa kwa majeshi ya Eritrea.

Katibu mkuu amesema hali ya sasa ya Ethiopia inaelekea kushindwa kudhibitiwa, vurugu zimefika kwenye kiwango cha kutisha, na muundo wa jamii sasa unaharibiwa.

Bw. Guterres amewambia wanahabari mjini New York kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kuunga mkono Umoja wa Afrika kwa kila njia inayowezekana kukomesha hali ngumu kwa waethiopia. Pia ametaka kurejeshwa kwa mazungumzo haraka iwezekanavyo ili kuleta suluhisho la kisiasa la kudumu, kwani hakuna suluhisho la kijeshi.