Tume tendaji ya wenyeviti ya mkutano mkuu wa CPC yakutana
2022-10-19 08:35:27| CRI

Tume tendaji ya wenyeviti(presidium) ya mkutano mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China jana ilikutana kwa mara ya pili chini ya uenyekiti wa Xi Jinping.

Kwenye mkutano huo, rasimu za maazimio ya ripoti ya kamati kuu ya 19 ya Chama, ripoti ya kazi za kamati ya 19 ya ukaguzi wa nidhamu ya Kamati kuu ya Chama, na marekebisho ya katiba ya Chama, zilipitishwa na kukabidhiwa kwa wajumbe wote wa mkutano mkuu ili zijadiliwe.

Naibu Katibu mkuu wa mkutano mkuu wa Chama Chen Xi ameiambia tume tendaji ya wenyeviti kuhusu majina ya wagombea waliopendekezwa na wajumbe mbadala wa kamati kuu ya 20 ya Chama, na wajumbe wa kamati ya 20 ya ukaguzi wa nidhamu ya kamati kuu ya Chama. Orodha ya majina hayo pia ilipitishwa, na kukabidhiwa kwa wajumbe ili ijadiliwe.