Mkutano wa nne wa pamoja na waandishi wa habari wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC wafanyika
2022-10-20 11:08:05| cri

Mkutano wa nne wa pamoja na waandishi wa habari wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umefanyika kwenye kituo cha habari cha mkutano huo.

Wasemaji saba wa ujumbe wa mji wa Chongqing, mikoa ya Sichuan, Guizhou, Yunnan, Shaanxi, Gansu na mkoa unaojiendesha wa Tibet wameeleza kuwa, wajumbe wamejifunza kwa makini ripoti ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama, na kuona kuwa ripoti hiyo imedhihirisha mwelekeo wa maendeleo ya Chama na taifa. Wajumbe wote wanaunga mkono ripoti hiyo na kueleza matumaini ya kufanya kwa bidii zaidi ili kuchangia katika ujenzi wa nchi ya kisasa ya kijamaa katika pande zote.