Kenya yazindua hatua za kuchochea ongezeko la sekta ya viwanda
2022-10-20 09:08:51| CRI

Kenya imezindua mpango wa kuchochea ongezeko kutokana na sekta ya viwanda.

Rais William Ruto wa Kenya amesema mjini Nairobi kuwa mpango wa asilimia 20 hadi mwaka 2030, ni mpango wa utekelezaji wenye lengo la kuongeza mchango wa sekta ya viwanda kwenye pato la taifa kufikia asilimia 20 kabla ya mwaka 2030, kutoka asilimia 7.2 ya sasa.

Rais Ruto amesema Kenya itapanua sekta yake ya viwanda kupitia kushauriana na kubadilishana mawazo na kwenda pamoja kama taifa.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanaviwanda ya Kenya (KAM) Bw. Rajan Shah, amesema kuna maeneo manne yenye fursa ya kuiwezesha Kenya kufikia lengo hilo, ambayo ni nguvu ya ushindani duniani, ongezeko linalolenga uuzaji nje wa bidhaa, kuifanya sekta ya kilimo kuhusiana na viwanda na kuendeleza makampuni madogo na yenye ukubwa wa kati.