Nchi za Afrika Kusini mwa Sahara ziko nyuma kutimiza malengo ya SDGs kuhusu maji na usafi
2022-10-20 09:07:29| CRI

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limesema nchi za Afrika Kusini mwa Sahara zimetajwa kuwa nyuma kwenye utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) kuhusu kushughulikia maji na usafi (WASH).

Akiongea kwenye kongamano la siku tatu kuhusu mwelekeo wa nchi za Afrika kwenye kutekeleza malengo hayo, naibu Mkurugenzi wa UNICEF nchini Ghana Bw. Fiachra McAsey amesema ni asilimia 65 tu ya watu katika eneo hilo wanapata huduma ya msingi ya maji, asilimia 33 wana mazingira ya kimsingi ya usafi, na mmoja kati ya watu watano anakosa vifaa vya usafi na kujisaidia maeneo ya wazi.

Amesema kuchelewa kufikiwa kwa malengo hayo, kunatokana na ukosefu wa fedha na kutokuwepo kwa uwekezaji wa kutosha.