UM watoa mwito wa kuchukua hatua za haraka kuhimiza amani nchini Sudan Kusini
2022-10-20 09:08:18| CRI

Umoja wa Mataifa umesema mgogoro wa Sudan Kusini unaendelea kuwa na utata wakati kiwango cha mateso kwa mamilioni ya watu kinaendelea kuwa hakivumiliki, na kutoa mwito wa kuchukuliwa kwa hatua za haraka ili kuhimiza amani.

Kamisheni ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imezitaka nchi za Afrika na wadau wengine kuonyesha uungaji mkono kwa utekelezaji wa makubaliano ya amani ya Sudan Kusini, nchi ambayo watu wake wanakabiliwa na msukosuko mkubwa wa kibinadamu lakini haufuatiliwi na vyombo vya habari.

Amesema kila mwezi maelfu ya watu wa Sudan Kusini wanavuka mpaka na wengine wanakimbilia maeneo ya ulinzi ya Umoja wa Mataifa ili kuepuka vurugu. Ameyataka mashirika ya misaada kuchangisha fedha kuwapa chakula watu wa huko, kwa sababu Sudan Kusini sasa haufuatiliwi kutokana na kuwepo kwa misukosuko mingine duniani.