Mkutano mkuu wa 20 wa CPC wapitisha marekebisho ya Katiba ya Chama
2022-10-23 13:40:10| CRI

Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) uliofungwa tarehe 22 hapa Beijing, umepitisha marekebisho ya Katiba ya Chama cha CPC, na kukubali kuyaongeza kwenye Katiba ya Chama, maendeleo mapya ya kinadharia katika Fikra ya Xi Jinping kuhusu Ujamaa wenye Umaalum wa China katika Zama Mpya tangu Mkutano Mkuu wa 19 wa CPC ufanyike, na kurekebisha na kuboresha maelezo kuhusu malengo ya kufikiwa kwenye Katiba kwa mujibu wa majukumu makuu ya CPC yaliyotajwa kwenye Mkutano Mkuu wa 20. Pia umebainisha malengo ya kimkakati ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii, ya kutimiza mambo ya kisasa ya ujamaa ifikapo mwaka 2035 na kuijenga China kuwa nchi ya kisasa ya ujamaa yenye nguvu ifikapo katikati ya karne hii, yaani kutimiza “Lengo la Pili la Juhudi za Miaka 100”.

Mkutano Mkuu umekubali kuyaongeza kwenye Katiba ya Chama majukumu makuu ya Chama yaliyotajwa kwenye mkutano huo kuhusu "kuendeleza ustawishwaji wa taifa la China katika nyanja zote kupitia njia ya China ya kujiendeleza kisasa". Umekubali kuyaongeza kwenye Katiba ya Chama kutimiza hatua kwa hatua lengo la ustawi wa pamoja kwa wote; kutumia wazo jipya la maendeleo yaliyo ya uvumbuzi, uratibu, kijani, uwazi, na pamoja; kuongeza juhudi za kukuza muundo mpya wa maendeleo unaozingatia uchumi wa ndani na unaoangazia mwingiliano mzuri kati ya mtiririko wa uchumi wa ndani na wa kimataifa; kuwapa jukumu kamili watu wenye vipaji kama rasilimali kuu; na kuhakikisha uchumi unaendelezwa kwa ubora wa juu, ufanisi zaidi, usawa, uendelevu, na usalama. 

Mkutano Mkuu umekubali kuongeza katika Katiba ya Chama kuendeleza demokrasia ya watu katika mchakato mzima; kuanzisha mifumo na taratibu nzuri za uchaguzi wa kidemokrasia, mashauriano ya kidemokrasia, kufanya maamuzi kwa demokrasia, usimamizi wa kidemokrasia na uangalizi wa kidemokrasia. Mkutano Mkuu umekubali kuweka kwenye Katiba ya Chama sera ya Nchi Moja, Mifumo Miwili; kupinga kwa uthabiti na kuwazuia wafarakanishaji wanaotaka "Taiwan ijitenge na China ".

Mkutano Mkuu umekubali kuweka katika Katiba ya Chama kuheshimu maadili ya pamoja ya binadamu ya amani, maendeleo, usawa, haki, demokrasia na uhuru; na kuendeleza ujenzi wa dunia yenye amani ya kudumu, usalama wa pamoja, na ustawi wa pamoja, uwazi na ujumuishi pamoja na usafi na mandhari nzuri. 

Pia umekubali kuyaongeza katika Katiba ya Chama majukumu makuu ya Chama kujisimamia kwa makini na kuhakikisha kuwa maafisa wa Chama hawana ujasiri, fursa, au hamu ya kuwa mafisadi.

Katiba ya Chama ni sheria kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, na ni mkusanyiko wa sifa, dhamira, matarajio makuu na malengo ya kufikiwa ya Chama, pamoja na nadharia na sera za mpango. Kwa mujibu wa mabadiliko ya hali ya ndani na nje ya nchi, Mkutano Mkuu wa CPC unaofanyika kila baada ya miaka mitano unafanya marekebisho ya katiba ili kuendana na wakati, jambo ambalo lina maana muhimu katika kuendeleza ujenzi wa Chama na kuongoza China kupata maendeleo katika shughuli mbalimbali.