Rais wa Tanzania kufanya ziara nchini China
2022-10-27 16:53:35| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi. Hua Chunying amesema rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya kitaifa nchini China kuanzia tarehe 2 hadi tarehe 4 mwezi Novemba kutokana na mwaliko wa rais Xi Jinping wa China.