Tamasha la maonyesho ya filamu za documentary za China lazinduliwa Afrika
2022-10-27 11:19:57| CRI

Tamasha la maonyesho ya filamu za documentary za China lilizinduliwa rasmi jana Jumatano barani Afrika, ambako filamu za documentary zinazoeleza “utawala wa China” kama vile “Kuongoza” “Kutegua Siri za Miaka Kumi” “Dhamira Kuu” zimeonyeshwa kwa watazamaji wa Afrika. Vituo vikuu vya televisheni vya Afrika vikiwa ni pamoja na vya Rwanda na Gabon vilitangulia kuonyesha filamu ya documentary "Kutegua Siri za Miaka Kumi” katika muda wa dhahabu.

“Tamasha la maonyesho ya filamu za documentary za China” linaandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya China. Afrika ni kituo cha kwanza cha maonyesho cha kikanda kwa Tamasha hilo, ambapo watu wa Afrika wanaweza kufahamu jinsi China inavyojiendeleza kisasa na kuanza safari mpya. Tamasha hilo linaweka jukwaa la kubadilishana mawazo juu ya kufikia makubaliano na kupanua ushirikiano kati ya China na Afrika. Maofisa wengi wa serikali za nchi za Afrika wametumia fursa hii kueleza matumaini yao mazuri wakisifu kwamba maendeleo mapya ya China yanatoa fursa mpya kwa dunia.

Mkuu wa CMG Bw. Shen Haixiong ametoa hotuba akisema wakati hali ya kimataifa inabadilika badilika, CMG itabeba majukumu yake ya kuwa vyombo vya habari, ili kuondoa vizuizi na kuzidisha maelewano kupitia njia ya utamaduni, na kujitahidi kuonyesha picha nzuri ya staarabu mbalimbali kuishi kwa masikilizano duniani.