Xi asisitiza kujitahidi kuwa na umoja katika kutimiza malengo yaliyowekwa na Mkutano Mkuu wa Chama
2022-10-28 09:38:53| CRI

Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Xi Jinping, amesisitiza kukuza moyo mkubwa wa waasisi wa chama na moyo wa Yan’an, na kujitahidi kuungana ili kutimiza malengo na kazi zilizowekwa na Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC.

Xi Jinping ambaye pia ni rais wa China na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi, Alhamis aliwaongoza wajumbe wengine sita wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC, kwenye ziara ya Yan’an ambayo ni kambi ya zamani ya mapinduzi mkoani Shaanxi Kaskazini Magharibi mwa China. Moyo wa Yan’an unasisitiza imani thabiti katika mwelekeo sahihi wa kisiasa, kanuni elekezi za kuweka huru akili na kutafuta ukweli ndani ya ukweli, kusudi la msingi la kutumikia watu kwa moyo wote na moyo wa ujasiriamali wa kujitegemea na kufanya kazi kwa bidii.