Xi asisitiza kujifunza, kuelewa na kutekeleza kwa kina moyo wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC
2022-10-28 09:45:52| CRI

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) mchana wa Oktoba 25 ilikutana kujifunza na kutekeleza moyo wa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC.

Akiongoza kikao hicho, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping, alisisitiza kuwa Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC umepata mafanikio makubwa katika siasa, nadharia na kazi za kiutendaji, na kuweka sera kubwa na mipango ya kimkakati ili kuboresha kazi ya Chama na nchi katika zama mpya.

Amesema moyo wa Mkutano huu unatumika kama tangazo la kisiasa na mpango wa hatua wa kujenga nchi ya ujamaa wa kisasa katika pande zote na kuongeza uhuishaji mkubwa wa taifa la China katika pande zote. Chama kizima lazima kijitahidi kujifunza kikamilifu, kuelewa na kutekeleza maudhui na kazi zilizowekwa na Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama na kujithidi kuleta mafanikio mapya katika kujenga nchi ya ujamaa wa kisasa katika pande zote.