Shughuli za CMG za kutangaza Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC zafanyika katika nchi mbalimbali barani Asia
2022-10-30 12:46:03| CRI

Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) lilifanya shughuli za kutangaza Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) katika nchi mbalimbali barani Asia zikiwemo Uturuki, Laos, Ufilipino na Nepal. Washiriki walifanya majadiliano ya kina kuhusu mada zilizohusu “Mambo ya kisasa ya Kichina”, “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, na “Safari Mpya ya China na Mustakabali wa Pamoja”.

Katika shughuli hizo, Hakan Okcal ambaye alikuwa balozi wa Uturuki katika nchi kadhaa amesema, chini ya uongozi wa CPC, watu maskini takriban 100 vijijini nchini China wameondokana na umaskini uliokithiri, na kiwango cha maisha ya wananchi kimeongezeka, hali iliyotoa mchango muhimu katika kulinda amani na utulivu na kuhimiza ukuaji wa uchumi duniani.

Naibu katibu wa Kamati ya Mkoa wa Luang Prabang ya Laos SuKanh Bounyong amepongeza mafanikio makubwa yaliyopatikana nchini China katika muongo uliopita kwenye zama mpya. Amesema pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja” limeleta fursa kubwa kwa maendeleo ya Laos. Reli kati ya Laos na China ambayo ilijengwa kwa ushirikiano na nchi hizo mbili imeleta faida halisi kwa watu wa Laos, na kuonesha moyo wa Jumuiya ya Mustakabali wa Pamoja kati ya nchi hizo mbili.

Vyombo vya habari zaidi ya 100 vya Uturuki, Laos, Ufilipino na nchi nyingine za Asia viliripoti na kutangaza moja kwa moja shughuli hizo.