Rwanda yasikitishwa na uamuzi wa DRC wa kumfukuza balozi wake nchini humo
2022-10-31 08:44:47| CRI

Serikali ya Rwanda imesema imesikitishwa na uamuzi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wa kumfukuza balozi wake nchini humo.

Jumamosi iliyopita, serikali ya DRC ilimwamrisha Balozi wa Rwanda nchini humo, Vincent Karega kuondoka nchini DRC ndani ya saa 48, kutokana na madai kuwa Rwanda inawaunga mkono waasi wa kundi la M23.

Hatua ilitangazwa na Msemaji wa Serikali ya DRC Patrick Muyaya baada ya kikao cha Kamati ya Ulinzi kilichoongozwa na rais wa nchi hiyo, Felix Tshisekedi, kilichofanyika baada ya kundi la M23 kudhibiti maeneo ya Kiwanja na Rutshuru katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Mara kwa mara DRC imekuwa ikiishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa kundi la M23, madai ambayo Rwanda imeyakanusha.