Mkutano wa kwanza wa Bunge la 6 la Afrika wafanyika nchini Afrika Kusini
2022-11-01 08:53:17| CRI

Mkutano wa kwanza wa kawaida wa Bunge la 6 la Afrika (PAP) umeanza jana mjini Johannesburg, Afrika Kusini, ambapo wabunge 257 wa Bunge hilo wanakutana ili kujadili masuala mbalimbali yanayoliathiri bara la Afrika.

Rais wa Bunge hilo Fortune Charumbira amesema, Afrika inakabiliwa na changamoto nyingi za vita ya wenyewe kwa wenyewe, mabadiliko ya serikali yasiyofuata katiba, ukosefu wa usalama wa chakula, umasikini, njaa, kuongezeka kwa mgogoro wa nishati na majanga ya asili, na kutoa wito kwa nchi za Afrika kukabiliana na changamoto hizo.

Amezitaka nchi za Afrika ambazo bado hazijaridhia Makubaliano ya Eneo la Biashara Huria la Afrika kufanya hivyo, na pia ametoa wito kwa nchi za Afrika kuondoa kwa haraka vizuizi vyote vya ushuru na vizuizi vingine ili kuwezesha usafirishaji huru wa watu na bidhaa katika bara hilo.