Baraza la Usalama la UM laongeza muda wa Tume ya Usaidizi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia
2022-11-01 08:57:25| CRI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limepitisha azimio na kuongeza muda wa Tume ya Usaidizi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia (UNSOM) hadi tarehe 31, mwezi Oktoba mwaka 2023.

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing amesema, China inaunga mkono kuongeza muda wa ujumbe wa UNSOM, lakini mswada wa azimio hilo bado unahitaji kuboreshwa kwenye masuala kadhaa ikiwemo kulinda raia, kuruhusiwa kwa misaada ya kibinadamu na kulinda watoto.