AU yatoa wito wa vijana kujumuishwa zaidi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Vijana
2022-11-02 08:41:34| CRI

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Afrika (AU) Moussa Faki Mahamat ametoa wito wa kujumuishwa zaidi kwa vijana, ikiwa ni katika maadhimisho ya Siku ya Vijana Afrika.

Amesema siku hiyo inayoadhimishwa Novemba Mosi, inaonesha umuhimu wa viongozi wa nchi za Afrika kuwashirikisha zaidi vijana, kama ilivyoanishwa kwenye dibaji ya Mkataba wa Vijana wa Afrika, ambao ni utajiri mkubwa wa bara hilo. Pia ameeleza umuhimu wa juhudi zinazotarajiwa za vijana wa bara hilo katika ushiriki na ujumuishi wao kwenye aina mpya ya maendeleo iliyoanza kutekelezwa na Umoja wa Afrika tangu Ajenda ya mwaka 2063 ilipotolewa mwaka 2013.

Bw. Mahamat amesema, vizuizi vingi vinawafanya baadhi ya vijana kutokuwa na mtazamo mzuri kwao binafsi, hatma zao, nchi zao pamoja na bara la Afrika, na kusisitiza kuwa, ushiriki na ujumuishi wa vijana unatoa chachu mpya katika majadiliano mbalimbali kupitia mawazo mapya.