Kenya yatoa dola za kimarekani milioni 16 kwa ajili ya kukabiliana na ukame
2022-11-02 08:46:05| CRI

Rais wa Kenya William Ruto amesema serikali yake imekusanya shilingi bilioni mbili, sawa na dola za kimarekani milioni 16.47, kutoa misaada ya chakula kwa kaunti zilizoathiriwa na ukame mkali zaidi nchini humo. 

Rais Ruto amesema serikali pia itashirikiana na wadau wa maendeleo na sekta ya binafsi kutafuta fedha za ziada ili kukabiliana na ukame.

Mamlaka ya Kitaifa ya Udhibiti wa Ukame (NDMA) imesema, idadi ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu imefikia milioni 4.35, kiasi ambacho kimeongezeka kutoka milioni 4.1 mwezi Juni.

Rais Ruto amesema ana imani kuwa juhudi zinazofanywa pamoja na wadau wa maendeleo na sekta ya binafsi zitaokoa maisha ya Wakenya katika maeneo yaliyoathiriwa zaidi na ukame.