China yasema ziara ya rais wa Tanzania itahimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili
2022-11-03 08:32:23| cri


 

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian jana kwenye mkutano na waandishi wa habari amesema, ziara ya rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania nchini China imeonesha urafiki na uaminifu kati ya nchi hizo mbili.

Amesema China ina imani kuwa ziara hiyo itahimiza uhusiano kati yao kuelekea kiwango cha juu zaidi.

Balozi wa Tanzania nchini China Mh. Mbelwa Kairuki hivi karibuni alisema, katika kipindi cha ziara ya rais Samia nchini China, nchi hizo mbili zitasaini makubaliano mengi ambayo yataleta fursa mpya kwa ushirikiano kati yao kwenye sekta za ujenzi wa miundombinu, kilimo, biashara na uwekezaji.