Ukraine yasema itarejea kwenye mazungumzo iwapo Russia itaondoa jeshi lake
2022-11-09 09:47:59| CRI

Mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak amesema Ukraine itarejea kwenye mazungumzo na Russia kama Russia itaondoa jeshi lake kutoka Ukraine.

Bw. Podolyak alipozungumza na gazeti la Italia La Repubblica amesema makubaliano ya kusitisha vita yanayoweza kufikiwa katika hali ya sasa ya mgogoro, yataipatia Russia nafasi ya kuimarisha nguvu yake. Pia amekanusha kuwa nchi za magharibi na Russia kufanya mazungumzo juu ya suala la Ukraine kama baadhi ya ripoti zilivyosema, yaani serikali ya Marekani na Wizara ya Ulinzi ya Russia wamejadili suala hilo.

Mgogoro kati ya Russia na Ukraine ulianzia tarehe 24 Februari mwaka huu na mazungumzo ya amani ya ana kwa ana ya hivi karibuni yalifanyika mwezi Machi.