Ubalozi wa China nchini Ethiopia waandaa tafrija kuwakaribisha wahitimu wa Ethiopia kutoka kwa vyuo vikuu vya China
2022-11-10 08:40:00| CRI

Ubalozi wa China nchini Ethiopia umeandaa tafrija kuwakaribisha wanafunzi wa Ethiopia waliohitimu kutoka kwenye vyuo vikuu vya China, wakati ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika elimu na mawasiliano ya kiutamaduni umepiga hatua kubwa katika miaka ya karibuni.

Kwa mujibu wa Ubalozi huo hafla hiyo imefanyika kuwakaribisha wahitimu ambao wameshuhudia ushirikiano kati ya China na Ethiopia unaoendelea kupanuka katika maendeleo ya raslimali watu, na vilevile maendeleo makubwa yaliyopatikana China katika miaka iliyopita.

Balozi wa China nchini Ethiopia Zhao Zhiyuan amesema, hafla hiyo inaonesha uungaji mkono kwa kuanzishwa kwa Mtandao wa Wahitimu wa Ethiopia kutoka kwenye Vyuo Vikuu vya China, ambao ulipendekezwa na wanafunzi waliorudi kutoka China.