Jeshi la Somalia lawaua wapiganaji 97 wa Al-Shabaab kwenye operesheni mbili
2022-11-10 08:40:33| CRI

Vikosi vya usalama vya Somalia vimewaangamiza wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi la Al-Shabaab kwenye operesheni mbili tofauti zilizofanyika katikati ya nchi hiyo.

Wizara ya Habari, Utamaduni na Utalii imesema, Jeshi la Taifa la Somalia SNA likiungwa mkono na wenyeji, limewaua wapiganaji 50 wa kundi la Al-Shabaab kwenye eneo la El Gorof jimboni Galgaduud, huku Shirika la Taifa la Intelijinsia na Usalama likiwaangamiza wapiganaji wengine 47 kwenye eneo la Basra.

Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa na Wizara hiyo mjini Mogadishu, serikali ya Somalia inashukuru wenyeji wa maeneo husika na washirika wa kimataifa waliochangia mafanikio ya operesheni hizi na kuvunja mitandao ya al-Shabaab ambayo ilikuwa inapanga mashambulizi dhidi ya umma.