WHO yachangia vifaa tiba kwa Nigeria kutokana na mafuriko makubwa
2022-11-11 08:56:47| CRI

Shirika la Afya Duniani WHO limetangaza kuwa limechangia vifaa tiba kwa jimbo la kusini la Nigeria la Anambra, kutokana na janga la mafuriko lililowaathiri watu laki 6 katika jimbo hilo.

Kwenye taarifa yake WHO imesema jimbo hilo lililoko kusini mwa Nigeria ni moja ya majimbo yaliyoathiriwa vibaya zaidi na mafuriko yaliyoyakumba zaidi ya majimbo 30 nchini Nigeria, na kufanya nyumba nyingi na vifaa vya afya kuzama kwenye maji, na kuathiri watu kisaikolojia.

Mratibu wa WHO katika jimbo hilo Bw. Adamu Abdulnasir amesema shirika hilo linafanya kazi na maofisa wa afya kutoa huduma za matibabu na kuimarisha ufuatiliaji.

Mwishoni mwa mwezi Oktoba serikali ya Nigeria ilisema watu 612 wamekufa na wengine milioni 3.2 wameathiriwa tangu msimu wa mvua wa mwaka huu uanze nchini Nigeria.