Rwanda yapunguza utoaji wa tani laki 1.26 za hewa ukaa katika miaka 9 iliyopita
2022-11-11 08:56:10| CRI

Rwanda imepunguza utoaji wa tani laki 1.26 za hewa ukaa katika kipindi cha zaidi miaka tisa iliyopita, kutokana na mkakati wake wa uwekezaji kwenye uhimilivu wa tabianchi katika nchi nzima.

Data zilizotolewa na Mfuko wa Kijani wa Rwanda kwenye mkutano wa 27 wa mabadiliko ya tabia nchi (COP27) unaoendelea nchini Misri, zinaonesha kuwa tangu mwaka 2013 jumla ya dola za kimarekani milioni 247 zimeelekezwa kwenye uwekezaji wa kimkakati wa uhimilivu wa tabianchi.

Fedha hizo zimewekezwa kwenye miradi 46 katika nchi nzima, eneo la hekta elfu 47 limepandwa misitu na hekta elfu 31 za maeneo ya maji zimehifadhiwa.

Hata hivyo waziri wa fedha wa Rwanda Bibi Claudine Uwera, amesema Rwanda inahitaji dola za kimarekani bilioni 11 ili kupunguza madhara na kuhimili mabadiliko ya tabianchi.