Mjumbe wa China atoa mwito kuunga mkono ujenzi wa uwezo wa nchi za Afrika wa kupambana na ugaidi
2022-11-11 08:38:18| CRI

Mjumbe wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Zhang Jun ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono ujenzi wa uwezo wa nchi za Afrika wa kupambana na ugaidi, ili kuondoa mizizi ya ugaidi.

Akiongea kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mapambano dhidi ya ugaidi barani Afrika, Balozi Zhang Jun amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuongeza nguvu ya kuunga mkono ujenzi wa uwezo wa kulinda usalama katika nchi za Afrika haswa kwenye nyanja dhaifu, kupitia kuzipatia misaada ya fedha, vifaa, upashanaji wa habari na ugavi.

Amesisitiza kuwa China itaendelea kufanya kazi pamoja na jumuiya ya kimataifa, kutumia ipasavyo fursa ya Pendekezo la Maendeleo Duniani, na kuongeza uungaji mkono kwa Afrika kwenye mapambano dhidi ya ugaidi, ili kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya kutimiza amani ya kudumu na maendeleo endelevu barani Afrika.