Sudan Kusini yalenga kupunguza vifo vya malaria kwa asilimia 80 ifikapo 2025
2022-11-11 09:15:25| CRI

Serikali ya Sudan Kusini imetangaza mipango ya kupunguza idadi ya vifo vinavyatokana na malaria kwa asilimia 80 ifikapo mwaka 2025.

Makamu wa rais wa nchi hiyo anayeshughulikia utumishi Bw. Hussein Abdelbagi Akol amesema kwenye ufungaji wa mkutano mmoja kuhusu ugonjwa huo huko Juba, kwamba sekta zote kwenye ngazi zote zinatakwa kuendelea kushirikiana katika kupambana na ugonjwa wa malaria.

Ripoti moja iliyotolewa mwaka jana na Shirika la Afya Duniani imeonyesha kuwa kila siku nchini humo watu takariban elfu 10 wanaambukizwa malaria huku watu 20 wakikufa kutokana na ugonjwa huo.