Matoleo ya Kiindonesia na Kithai ya dokumentari kuhusu misemo ya kale ya Kichina iliyonukuliwa na Xi yalizinduliwa
2022-11-15 10:02:52| CRI

Matoleo ya Kiindonesia na Kithai ya filamu ya dokumentari kuhusu misemo ya kale ya Kichina iliyonukuliwa na Rais Xi Jinping wa China yalitangazwa nchini Indonesia na Thailand kuanzia Jumatatu.

Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG lilishirikiana na vituo viwili vya televisheni nchini Indonesia na Thailand kutengeneza dokumentari inayowasilisha misemo ya kitamaduni na hadithi za kitamaduni ambazo Xi alinukuu.

Pia siku hiyo ya Jumatatu, dokumentari ya "China kwenye Safari Mpya," iliyotafsiriwa kwa lugha mbalimbali inayohusu harakati za China za kutafuta nchi ya kisasa, ilianza kuonyeshwa kwa mara ya kwanza kwenye televisheni katika nchi zikiwemo Thailand, Cambodia, India, Laos, Nigeria, Pakistan, Sri Lanka na Uturuki.