Bibi Peng Liyuan asema watu wa China na Thailand wana maadili sawa
2022-11-18 21:36:23| cri
Mke wa rais wa China Bibi Peng Liyuan, ametembelea Makumbusho ya taifa ya Sanaa ya Ayutthaya huko Ayutthaya, Thailand, makumbusho ambayo pia yametembelewa na wake wa baadhi ya viongozi waliohudhuria Mkutano wa 29 wa Viongozi wa Kiuchumi wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia-Pacific (APEC).
Mke wa Waziri mkuu wa Thailand Bibi Naraporn Chan-o-cha alimkaribisha Bibi Peng na kuambatana naye kwenye wakati wa ziara nzima. Kwenye maonesho hayo kazi za sanaa kwa ajili ya sherehe kuu za familia ya Kifalme ya Thailand na kazi za mikono za kitamaduni za Thailand zinaonesha. Bibi Peng alisikiliza maelezo kuhusu sanaa hizo, na kusifu ufundi na mbinu za mafundi wa Thailand.
Bibi Peng pia amepongeza kuwa maonyesho pia yanaendana na dhana ya China ya kupunguza umaskini katika maeneo ambayo hayajaendelea. Pia aliahidi kuwa atanunua baadhi ya kazi zao kusaidia miradi ya kupambana na umaskini ya familia ya Kifalme ya Thailand. Bibi Peng pia alizungumzia kufanana kwa mambo kati ya wachina na watu wa Thailand, akisema wachina wanapenda mayunguyungi na wanathamini ubora wake. Bibi Naraporn alikubali na kusema mayungiyungi hutumiwa kutoa heshima kwa Buddha na watu wa Thailanda. Peng alisema kwa mara nyingine tena hii inaonyesha kuwa watu wa China na Thai wana maadili yanayofanana