Xi atoa wito wa biashara huria na ya kufungua mlango katika mkutano wa viongozi wa kiuchumi wa APEC
2022-11-19 21:04:36| cri

Rais Xi Jinping wa China amesema biashara huria na ya kufungua mlango na uwekezaji ni miongoni mwa madhumuni na kanuni za Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia na Pasifiki (APEC) na nguzo muhimu katika utekelezaji wa Dira ya Putrajaya 2040.

Xi aliyasema hayo leo Jumamosi alipoendelea kuhudhuria Mkutano wa 29 wa Viongozi wa Kiuchumi wa APEC, uliojikita katika majadiliano kuhusu biashara endelevu na uwekezaji. Rais Xi alisisitiza umuhimu wa kushikilia utaratibu halisi wa pande nyingi na kulinda mfumo wa biashara wa pande nyingi, kudumisha ujumuishi kwa manufaa ya wote, kudumisha ushirikiano wazi wa kikanda kwa ajili ya ustawi wa Asia na Pasifiki.

Mkutano huo ulitangaza Azimio la Viongozi wa Kiuchumi wa APEC wa 2022 na Malengo ya Bangkok kuhusu Uchumi wa Kijani wa Mzunguko wa Biolojia.