Xi apongeza kufunguliwa kwa Semina ya Wenzi wa Kimataifa wa UM na China kuhusu Utafiti wa Anga ya Juu na Uvumbuzi
2022-11-21 20:29:04| cri

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya kupongeza Semina ya Uhusiano wa Wenzi wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa na China kuhusu Utafiti wa Anga ya Juu na Uvumbuzi ambao umefunguliwa leo mjini Haikou, mkoani Hainan, kusini mwa China.

Rais Xi amesema China inapenda kuongeza mawasiliano na ushirikiano na nchi mbalimbali, kutafiti siri za anga ya juu kwa pamoja, kutumia kwa amani anga ya juu, na kuhimiza teknolojia za safari za anga ya juu kunufaisha watu wa nchi mbalimbali duniani.