China yaagiza kambakoche hai kutoka Kenya
2022-11-21 08:56:27| CRI

Ndege iliyobeba kilo 404 za kambakoche hai kutoka Nairobi, Kenya, ilitua Alhamisi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Changsha Huanghua, ikiwa ni shehena ya kwanza ya bidhaa kama hizo iliyoagizwa kutoka Kenya hadi Mkoa wa Hunan, China, mwaka huu.

Baada ya kuwekwa karantini katika Forodha ya Changsha, bidhaa hizo zitaingia kwenye soko la China hivi karibuni.

Kwa mujibu wa mwagizaji wa China wa bidhaa hizo, kamba za Kenya zina bei nafuu kuliko zinazoagizwa kutoka Australia, na anapanga kupanua uagizaji wake ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wa China.

Forodha ya China imefungua njia ya haraka kwa bidhaa za baharini zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.