Rais wa Tanzania aamuru utafiti wa kina ufanyike kutokana na uharibifu wa mazingira katika maziwa makuu matatu mkoani Manyara
2022-11-24 08:55:14| CRI

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameamuru utafiti wa kina ufanyike ili kujua chanzo kilichosababisha uharibifu wa mazingira katika maziwa matatu makubwa yaliyoko mkoa wa Manyara, kaskazini mwa nchi hiyo.

Rais Samia ameliamuru Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira kufanya utafiti huo mapema katika Ziwa Babati, Ziwa Basotu na Ziwa Manyara, ambayo yanakabiliwa na uchafuzi wa mazingira.

Pia rais Samia ameeleza kuanzishwa kwa kampeni za kupanda miti karibu na maziwa hayo ili kuyalinda yasiharibiwe zaidi.