UNECA yazitaka nchi za Afrika kuimarisha biashara ya ndani kukabiliana na mishtuko kutoka nje
2022-11-25 08:34:20| CRI


 

Kaimu katibu mkuu wa Tume ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) Antonio Pedro amesisitiza haja ya nchi za Afrika kuboresha biashara ya ndani ili kukabiliana na mishtuko kutoka nje.

Akizungumza katika Baraza la Ngazi ya Juu la Umoja wa Afrika lililofanyika mjini Niamey, Niger, Pedro amesema Afrika inayofanya biashara kubwa ya ndani katika bidhaa za aina mbalimbali ni chaguo bora zaidi katika kujenga Afrika yenye unyumbufu inayoweza kuvumilia changamoto zinazotoka nje ya bara hilo.

Amesema bara la Afrika limepata changamoto kubwa kuliko maeneo mengine kutokana na janga la COVID-19 na athari za mgogoro nchini Ukraine, na hii inatokana kwa kiasi kikubwa na utegemezi wake wa kuagiza bidhaa nje. Pia amesisitiza kuwa mageuzi endelevu ya kiuchumi ya Afrika yanahitaji ukuaji wa viwanda endelevu na unaoharakishwa.