DRC kufanya uchaguzi wa urais Desemba 2023
2022-11-28 09:43:02| CRI

Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (CENI) imetangaza kuwa uchaguzi ujao wa rais wa nchi hiyo utafanyika tarehe 20 mwezi Desemba 2023.

Tangazo hili lilitolewa wakati wa sherehe rasmi iliyoandaliwa Jumamosi mjini Kinshasa na mwenyekiti wa tume hiyo Bw. Denis Kadima, ambaye pia alitangaza ratiba za uchaguzi wa wabunge, mikoa na mitaa.