WFP yapunguza msaada wa chakula kwa Sudan kutokana na ukosefu wa fedha
2022-12-01 09:02:52| CRI

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limetangaza kupunguza msaada wa chakula kwa Sudan kutokana na ukosefu wa fedha.

WFP limesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa kupunguza msaada kwa Sudan kunaathiri matibabu ya kuokoa maisha na kuongeza hatari ya utapiamlo na uwezekano wa vifo kwa asilimia 50 kati ya watoto milioni 1.7 walio na utapiamlo mkali.

Shirika hilo limesema linahitaji karibu dola za kimarekani milioni 7  kuendelea na shughuli zake kama kawaida hadi mwisho wa mwaka huu.