UM yaanza kuchunguza vurugu zilizofanywa na M23 dhidi ya raia nchini DRC
2022-12-07 09:25:36| CRI

Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, Bibi Stephanie Tremblay jana alisema, tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo MONUSCO imeanza kufanya uchunguzi wa haki za binadamu juu ya vurugu zilizofanywa na kundi la M23 dhidi ya raia.

Alisema Ofisi ya Haki za Binadamu ya UM na MONUSCO zitashirikiana katika kuchunguza mapambano kati ya kundi la M23 na jamii ya Mai-Mai huko Kishishe, Rutshuru. Timu hiyo inawahoji mashuhuda na wahanga huko Kishishe iliyoko chini ya udhibiti wa kundi la M23. Vikosi vya tume hiyo viliwaondoa raia wanaotaka kutafuta hifadhi kwenye kambi ya MONUSCO iliyoko Rwindi.

Msemaji huyu aliongeza kuwa MONUSCO inatoa wito wa kusitisha mapambano na kuunga mkono kikamilifu mapendekezo ya kikanda katika kutimiza amani.