Xi ajibu barua ya wanafunzi wanaojifunza Kichina nchini Saudi Arabia
2022-12-08 09:31:37| CRI

Rais Xi Jinping wa China hivi karibuni alijibu barua ya  wajumbe wa wanafunzi wanaojifunza lugha ya Kichina nchini Saudi Arabia, akiwahimiza vijana wa nchi hiyo kujifunza Kichina vizuri na kutoa mchango mpya katika kuimarisha urafiki kati ya China na Saudi Arabia na China na nchi za Kiarabu.

Kwenye barua yake, rais Xi amebainisha kuwa lugha ni ufunguo bora wa  kuijua nchi moja, na anafurahi kwa dhati kwamba vijana wameijua China ni nchi yenye rangi na sura mbalimbali kwa kupitia kujifunza Kichina na kushiriki katika mpango wa “Daraja la Kichina”. Ameongeza kuwa hivi sasa, Watu wa  China na watu wa Saudi Arabia wanafanya bidii kutimiza ndoto zao kuu, ambapo kujifunza lugha na kuelewa historia na utamaduni wa upande mwingine kutasaidia kukuza maelewano na kujenga uhusiano wa karibu kati ya watu wa nchi hizo mbili, na pia kuchangia ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye  mustakabali wa pamoja.