Xi awasili Riyadh kuhudhuria Mikutano ya kilele na Nchi za Kiarabu
2022-12-08 09:30:44| CRI

Rais Xi Jinping wa China amewasili nchini Saudi Arabia Jumatano alasiri na kuhudhuria mkutano wa kwanza wa wakuu wa China na nchi za Kiarabu na Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na nchi za Kiarabu za Ghuba (GCC),   na pita atafanya ziara ya kiserikali nchini Saudi Arabia kutokana na mwaliko wa Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saudi Arabia.

Baada ya kulakiwa kwa furaha na  watu wa Saudi Arabia kwenye uwanja wa ndege, Xi alitoa  hotuba ya maandishi,  akiwa kwa niaba ya serikali na watu wa China, alitoa salamu na kuitakia kila heri serikali na watu wa Saudi Arabia. Amesema China na Saudi Arabia zimezidi kuaminiana kimkakati, na  ushirikiano wa kivitendo kati ya nchi hizo mbili katika  sekta mbalimbali umepata matokeo mazuri tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia miaka 32 iliyopita.

Akibainisha kwamba hasa tangu kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimkakati wa kina kati ya China na Saudi Arabia mwaka 2016, Xi amesema yeye na Mfalme Salman wameshirikiana pamoja  na kuelekeza uhusiano wa nchi hizo  kupata maendeleo makubwa, ambayo si tu kwamba  yamewanufaisha watu wao, bali pia  yamechangia amani, utulivu, ustawi na maendeleo ya kikanda.