Xi akutana na marais na viongozi wa nchi mbalimbali za kiarabu mjini Riyadh
2022-12-09 09:30:24| CRI

Rais Xi Jinping wa China jana alikutana na marais na viongozi wa nchi mbalimbali za Kiarabu huko Riyadh.

Alipokutana na rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi, rais Xi ameeleza kuwa kadiri mazingira ya kikanda na kimataifa yanavyoendelea kuwa na mabadiliko makubwa na yenye utata, umuhimu wa kimkakati na wa jumla wa uhusiano kati ya China na Misri umedhihirika zaidi. Maono na maslahi waliyonayo China na Misri yanamaanisha kuwa pande hizo mbili zinahitaji kushirikiana katika kujenga jumuiya ya China na Misri yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya, na kuendeleza zaidi ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Misri.

Kwa upande wake rais Sisi amesema Misri inafurahia kuwa na rafiki mkubwa kama China na inatarajia kuimarisha zaidi ushirikiano wo wa kimkakati wa kina na kukuza ushirikiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali ili kuleta matokeo mazuri zaidi.

Aidha alipokutana na rais wa Palestina Mahmoud Abbas rais Xi amebainisha kwamba urafiki kati ya China na Palestina unathaminiwa sana na watu wake, na kuongeza kuwa katika miongo mitano iliyopita na zaidi pande hizo mbili zimekuwa zikiaminiana na kusaidiana, ambapo rais Abbas kwa upande wake alisisitiza tena kuwa Palestina inaendelea kushikilia kanuni ya China moja na kuunga mkono kwa dhati msimamo wa haki wa China katika masuala yanayohusiana na Taiwan, Hong Kong na Xinjiang.

Wakati huohuo alipokutana na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan, rais Xi amesema China inaunga mkono pande zote nchini Sudan kuendelea kusukuma mbele mabadiliko ya kisiasa kwa njia ya mazungumzo na mashauriano, na kupinga majeshi ya nje kuingilia katika masuala ya ndani ya Sudan, ambapo pia itaendelea kutetea marafiki wa Sudan katika jukwaa la kimataifa.