Sudan Kusini yatangaza mlipuko wa surua
2022-12-12 09:02:04| CRI

Sudan Kusini imetangaza mlipuko wa ugonjwa wa Surua kutokana na kuongezeka kwa kesi zilizothibitishwa kuwa na ugonjwa huo katika wiki 38 za maambukizi zilizopita.

Mkurugenzi Mkuu wa Huduma za Udhibiti wa Afya katika Wizara ya Afya nchini humo John Rumunu amesema, watu 31 wamefariki na wengine 2,471 wamethibitishwa kuwana ugonjwa huo katika kaunti zote nchini Sudan Kusini.

Amesema nchi hiyo imeshuhudia milipuko ya mara kwa mara ya Surua tangu mwaka jana, hasa kutokana na kuvurugika kwa utaratibu wa utoaji wa chanjo na utekelezaji hafifu wa shughuli zinazoendana na utoaji wa chanjo.

Ameongeza kuwa, kampeni ya mwisho ya chanjo ya surua ilifanyika nchini Sudan Kusini mwaka 2020, huku chini ya asilimia 85 wakipata chanjo hiyo, ambayo ni chini ya lengo lililopendekezwa la asilimia 95.