Polisi wagundua maiti 27 za raia wa kigeni katika mji mkuu wa Zambia
2022-12-12 08:40:21| CRI

Polisi wa mjini Lusaka, Zambia, wamegundua maiti 27 za watu wanaoshukiwa kuwa raia wa kigeni zilizotupwa na watu wasiojulikana.

Naibu Msemaji wa polisi Bw. Danny Mwale amesema, maiti hizo zinazoshukiwa kuwa ni za raia wa Ethiopia, ziligunduliwa na wananchi jana alfajiri katika eneo la Ngwerere, pembezoni mwa mji mkuu wa Zambia, Lusaka.

Bw. Mwale amesema, mbali na maiti 27, raia mmoja wa kigeni alikutwa akiwa mahututi na kupelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.