Rais wa Sudan Kusini azindua barabara ya kisasa iliyojengwa na China
2022-12-13 08:52:52| CRI

Rais wa Sudan Kusini Bw. Salva Kiir jana jumatatu amezindua sehemu ya barabara mpya ya Juba-Terekeka yenye urefu wa kilomita 63 ambayo ujenzi wake umekamilika, ikiwa ni sehemu ya barabara kuu ya Juba-Rumbek yenye urefu wa kilomita 392 inayojengwa na Kampuni ya China ya SDHS.

Barabara hiyo itaunganisha jimbo la Equatoria ya Kati na majimbo mengine sita ya nchi hiyo.

Rais Kiri amesema, barabara hiyo ya kisasa itawanufaisha wakulima na wafanyabiashara kupitia usafirishaji wa  mazao ya kilimo na bidhaa za viwandani hadi sokoni. Pia ameishukuru serikali ya China kwa ushirikiano kati yao katika ujenzi wa barabara hiyo.