Watalii wa kigeni waongezeka kwa kasi nchini Tanzania
2022-12-14 10:07:49| CRI

Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi katika Mamlaka ya Takwimu nchini Tanzania Daniel Masolwa amesema, idadi ya watalii wa kigeni waliotembelea nchi hiyo kati ya Januari na Oktoba mwaka huu imeongezeka kwa asilimia 64 ikilinganishwana mwaka jana kipindi kama hicho.

Masolwa amesema kati ya mwezi Januari hadi Oktoba mwaka huu, watalii 1,175,697 wa kigeni walitembelea Tanzania ikilinganishwa na watalii 716,741 katika kipindi kama hicho mwaka 2021. Amebainisha kuwa ongezeko la watalii wa kigeni linatokana na juhudi za serikali zinazolenga kufufua sekta ya utalii baada ya janga la COVID-19.