Kampuni ya China yatoa nafasi 5,000 za fursa kwa Wakenya kupitia maonyesho ya ajira
2022-12-16 09:05:48| CRI

Maonyesho ya siku tatu ya ajira yaliyoandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya simu ya China, Huawei, yameanza jana alhamis katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, ili kusaidia kutoa fursa za ajira.

Katika maonyesho hayo yaliyokutanisha zaidi ya waajiri 100 wanaohitaji watu wenye ujuzi na uwezo mdogo kwa ajili ya ajira na fursa za mafunzo kazini, kampuni ya Huawei ilitangaza kuwa itatoa fursa 5,000 za ajira.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa maonyesho hayo, Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua alisema maonyesho hayo na shughuli nyingine kama hizo zinachukua nafasi kubwa katika fursa za ajira, kubadilishana maoni na uzoefu na pia kuisukuma Kenya kuwa kitovu cha fursa za ajira.

Naye naibu mkurugenzi mkuu wa Masuala ya Umma wa kampuni ya Huawei tawi la Kenya, Steven Zhang amesema, maonyesho ya ajira yanaonyesha nguvu ya nchi, ujasiri wa Wakenya na pia matarajio mazuri kati ya wafanyabiashara wa Kenya.