Benki ya Kenya yakamilisha ununuzi wa Benki ya Trust Merchant ya DRC
2022-12-16 09:11:02| CRI

Benki ya Biashara ya Kenya (KCB), imesema imekamilisha ununuzi wa Trust Merchant Bank (TMB) yenye makao yake nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya kutimiza vigezo vyote vinavyotakiwa.

Katika taarifa yake iliyotolewa mjini Nairobi, Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Paul Russo amesema Benki hiyo imepata vibali vya udhibiti kutoka Kenya, DRC, na Tume ya Ushindani ya Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA), na hivyo kuweka mazingira kwa KCB  kupata asilimia 85 ya hisa za TMB.