Peru yatangaza hali ya hatari kutokana na maandamano yaliyosababisha vurugu
2022-12-16 07:58:12| CRI

Peru imetangaza hali ya hatari kwa siku 30 nchini humo kwa lengo la kuzima maandamano yanayosababisha ghasia katika mikoa mbalimbali nchini humo.

Waziri wa Ulinzi wa nchi hiyo Alberto Otarola amesema hayo baada ya kikao cha Baraza la Mawaziri, na kuongeza kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na wizi na vurugu, na kufungwa kwa barabara kuu na za mitaa, vitendo ambavyo amesema vinadhibitiwa na Jeshi la Polisi na Jeshi la Ulinzi la nchi hiyo.

Machafuko ya kisiasa nchini Peru yamesababishwa na kuondolewa madarakani kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Desemba 7, na yameenea kutoka sehemu ya kusini mwa nchi hiyo katika miji iliyo kaskazini.