Mkuu wa UNECA azitaka nchi za Afrika kubadilisha changamoto zinazojitokeza kuwa fursa
2022-12-16 07:59:38| CRI

Kaimu katibu mtendaji wa Kamati ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa (UNECA) Bw. Antonio Pedro amezitaka nchi za Afrika kubadilisha changamoto zinazojitokeza za kiuchumi na kimazingira kuwa fursa kwa kuanzisha ushirikiano imara na mikakati ya kibunifu.

Bw. Pedro amesema hayo kwenye Maonyesho ya siku tatu ya UNECA, yanayofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha UNECA huko Addis Ababa, Ethiopia. Pia amesisitiza haja ya maendeleo ya haraka ya teknolojia na uwekezaji wa kidijitali wa uchumi barani Afrika ili kukabiliana na matatizo yaliyopo.