Watu 20 wafariki kwa kipindupindu kusini mwa Nigeria
2022-12-19 09:03:06| CRI

Ofisa wa jimbo la Cross River kusini mwa Nigeria amesema mlipuko wa kipindupindu uliotokea katika jimbo hilo umesababisha vifo vya watu wasiopungua 20.

Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Afya ya Msingi la Cross River Bibi Janet Ekpeyong, amewaambia waandishi wa habari kuwa viongozi wa eneo hilo wameanzisha uchunguzi kuhusu mlipuko huo uliorekodiwa katika vijiji 10 kwenye eneo la Abi kati ya Alhamisi na Jumamosi.

Bibi Ekpeyong amesema hadi sasa watu zaidi ya 30 wamelazwa hospitali kutokana na ugonjwa huo, na serikali ya jimbo hilo imetuma watu na rasilimali katika vijiji vilivyoathirika ili kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa huo.