Rais wa Afrika Kusini ahimiza ushirikiano na kutokomeza rushwa
2022-12-21 08:48:02| CRI

Rais wa Afrika Kusini na mwenyekiti wa chama tawala nchini humo cha African National Congress (ANC) Cyril Ramaphosa, amewataka wanachama wote wa ANC waliochaguliwa, kuitumikia nchi hiyo na kuchukua hatua zote zinazohitajika kukomesha ufisadi.

Akiongea kwenye ufungaji wa mkutano wa 55 wa ANC ulioanza tarehe 16 na kumaliza jana, Rais Ramaphosa amesema majadiliano ndani ya ANC yameonyesha msimamo thabiti dhidi ya ufisadi. Amesema rushwa ndani ya ANC ni tishio kubwa kwa uhai wa ANC na kwa mustakabali wa mapinduzi ya kitaifa ya kidemokrasia. Amesema mapambano dhidi ya ufisadi yanaweza kupingwa na kuongeza mifarakano ndani ya ANC, lakini mkutano huo umetambua kuwa hakuna chaguo lingine bali ni kupambana na ufisadi au kuteketea.