China na Zambia zaahidi kuimarisha ushirikiano katika kilimo na biashara ndogo na zenye ukubwa wa kati (SMEs).
2022-12-22 08:56:07| CRI

China na Zambia zimesisitiza kuimarisha ushirikiano katika sekta ya kilimo na sekta ya biashara ndogo na zenye ukubwa wa kati (SMEs).

Balozi wa China nchini Zambia Bw. Du Xiaohui na Waziri wa Maendeleo ya Biashara Ndogo na zenye ukubwa wa kati wa Zambia Bw. Elias Mubanga, wametoa ahadi hiyo kwenye mkutano uliofanyika mjini Lusaka.

Balozi Du amesema China inapenda kushirikiana na Zambia kuvumbua mifano ya ushirikiano katika kilimo na sekta nyingine na kuchochea uhai wa makampuni kwa kuimarisha ushirikiano.

Bw. Mubanga amesema serikali ya Zambia inathamini mawasiliano na ushirikiano na China, na inatarajia kuimarisha ushirikiano na China katika sekta ya kilimo na biashara ndogo na zenye ukubwa wa kati.