Sehemu ya kwanza ya mradi wa Hifadhi ya Viwanda ya PK24 iliyojengwa na kampuni ya China nchini Côte d'Ivoire yakamilika.
2022-12-26 08:41:32| cri

Sehemu ya kwanza ya mradi wa Hifadhi ya Viwanda ya PK24 nchini Cote d'Ivoire iliyojengwa na kampuni ya China (China Harbour Engineering Co. Ltd.) ilikamilika tarehe 23 Disemba.

Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye hafla ya kukamilika kwa mradi huo, Waziri Mkuu wa Côte d'Ivoire Patrick Asch alisema , mradi huo utahimiza mageuzi ya kiuchumi ya Côte d'Ivoire na kuingiza nguvu mpya katika ujenzi wa viwanda wa nchi hiyo.

Meneja mkuu wa kanda ya Afrika Magharibi wa kampuni hiyo Bw. Wang Guangsheng, alisema wafanyakazi wa ujenzi wa mradi huo wengi ni wenyeji ambao walipewa mafunzo mazuri. Ameongeza kuwa mradi huo umezingatia ubora wa mradi na udhibiti wa usalama, ambao ulisifiwa na serikali ya nchi hiyo.